WATOTO KATAVI WATAKIWA KULELEWA MAADILI YA KUITUMIKIA TANZANIA

Waislam katika sgerehe za Eid Elfitri Mjini Mpanda

Wa nne kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi akishiriki Ibada ya Eid Elfitri Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mjini Mpanda

NA.Issack Gerald-Katavi
Jamii Mkoani Katavi imetakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kuwatumikia watanzania katika utumishi wa umma wanapokuwa wakubwa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr.Ibrahimu Msengi katika sherehe za Idi El Fitri ambazo zimeandaliwa na Umoja Balaza la Wanafunzi Vijana wa Kiislamu Mkoani Katavi katika viwanja vya Shule ya Sekondari Istqama iliyopo Mjini Mpanda.
Adha Msengi amewashauri  watu wote ndani na nje ya Mkoa wa Katavi waliohitmu masomo yao na kupata ajira baada ya kusomeshwa na wazazi,walezi ,ndugu ,jamaaa na Marafiki zao kurejea kuwekumbuka kwa kuwasaidia katika mahitaji wanayoyahitaji.
Katika sherehe hizo ,Mkuu huyo wa Mkoa ametoa shilingi milioni moja kwa balaza hilo la wanafunzi wa kiislamu kwa ajili kutumia katika mahitaji ya kuendesha umoja wao.
Sherehe hii pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu kutoka Dar es Salaam.

Kwa upande wake Shekhe wa balaza la waislam Mkoa wa Katavi Shekhe Nassoro Kakulukulu amewataka waislamu wote kuendlea kuitunza na kuienzi amani iliyopo Tanzania bila kujali itikadi za dini na siasa.
Sherehe za Idd El Fitri ni sherehe ambazo husherehekewa mara baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani kumalizika

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA