MKUU WA JESHI TANZANIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA ZAHANATI YA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya Jeshi la Polisi Mkoani Katavi.
Katika taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilayani Mpanda Maria Kwayi,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 7 zimekwishatumika katika ujenzi ambapo inahitajika zaidi ya shilingi milioni 29 ili jengo likamilike huku changamoto ikiwa ni upungufu wa vifaa vya ujenzi.
Kwa upande wake IGP sirro mara baada ya kupokea taarifa hiyo amesema jeshi la polisi litaongeza takribani milioni kumi na Tano ili kuunga juhudi za ujenzi wa zahanati hiyo.
Wakati huo huo IGP siro aliyehitimisha ziara yake jana Mkoani Katavi amesema,wafanyabiashara Mkoani Katavi,Jeshi la Polisi Mkao makuu na serikali kuu wataangazia hatua za haraka ili zipatikane nyumba kwa ajili ya polisi ili kutatua uhaba wa nyumba za polisi Mkoani Katavi.
IGP Simon Sirro alikuwa na ziara ya kikazi siku mbili juzi na jana Mkoani katavi akitokea Mkoani Kigoma kabla ya kuelekea Mkoani Rukwa.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA