WASITISHA SAFARI ZA KUSAFIRISHA ABIRIA KATAVI KWENDA MIKOANI

Miongoni wa wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamesitisha huduma kutokana na ubovu wa miundombinu.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji wanaomiliki mabasi ya mikoani ambazo zinatumia barabara inayoanzia Mpanda kuelekea Tabora tabora.
Magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya Mpanda-Tabora yamepewa utaratibu wa kutumia barabara ya Mpanda-Kigoma au Mpanda-Mbeya ambapo wafanyabiashara wengine wamesema wanalazimika kuongeza nauli kwa shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa safari umeongezeka
Hata hivyo kwa mjibu wa wasafirishaji hao wamesema barabara mbadala ya kupitia Uvinza Mkoani Kigoma nayo haipo katika hali nzuri kitendo kinachosababisha ugumu wa safari.
Jumamosi ya Aprili 16,2018,mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mwishoni mwa wiki iliyopia mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela alikuwa amesema kutokana na barabara ya Mpanda-Tabora kuharibika kwa kiasi kikubwa watawapatia waraka wa mwongozo wa safari ili wenye mabasi wasafirishe abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya.
Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA