MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA KWA KUMILIKI RISASI ZA SILAHA YA KIVITA

Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa hukumu dhidi ya Bw.Kigalu Huba(25) mkazi wa kijiji cha Kambuzi wilayani Mpanda Mkoani Katavi aliyekuwa akituhumiwa kwa kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha AK-47 ya kivita ambapo mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 20.
Hakimu mkazi wa mahakama  hiyo Mh.Chiganga Tengwa akitoa hukumu hiyo leo amesema mahakama imejiridhisha bila kuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo baada ya kusikiliza shadi wa pande zote ambazo ni mtuhumiwa na upande wa Jamhuri ambao ni serikali.
Awali upande wa Jamhuri ambayo ni serikali wamesema Bw. Kigalu Huba  alikutwa na risasi hizo Machi 19,2018 ambapo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 7 ya mwaka 2015 kinachohusu umiliki wa silaha  huku wakiiomba Mahakam itowe adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe wenye tabia kama hiyo.
Kwa upande wake Bw.Huba akitoa utetezi wake mahakamani hapo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu aliyopewa akisema kuwa anategewa ana mke na watoto watatu na asipopunguziwa adhabau hiyo familia yake itaathirika.
Aidha katika maelezo ya mtuhumiwa ni kuwa risasi hizo hazikuwa zake bali zilikuwa na mwananchi mwingine ambaye amemtaja kwa jina moja la Shimangu anayeishi katika kijiji ambacho yeye Bw.Kigalu Huba hakifahamu kwa kuwa walikuwa wanakutana miataani.
Mara baada ya utetezi huo baada ya mahakama imejiridhisha kujirisha bila shaka kuwa ni mtuhumiwa alitenda kosa hilo ambapo hakimu Mh.Chgangwa Tengwa kwa kuzingatia kifungu cha 235(1) ya mwenendo ya makosa jinai sheria namba 20 ya mwaka 2002 amemhukumu kwenda jera miaka 20 kuanzia Aprili 10,2018.
Kwa mjibu wa hukumu hiyo,mtuhumiwa ana nafasi ya kukata rufaa ikiwapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa dhidi yake kutokana na mashtaka yanayomkabili.
Nao baadhi ya wananchi kutoka kijiji cha Kambuzi walikuwa wamehudhuria ili kufahamu hatima ya kesi ya Bw.Kigalu Huba ambaye wamekuwa wakimtuhumu kuwa tishio kwa wananchi kwa kujihusisha na uharifu.
Katika kesi hiyo Mashuhuda wapatao wane walihudhuria kutoa ushahidi akiwemo mkuu wa upelelezi kutoka jeshi la Polisi Mkoani Katavi Emmanuel Parangyo,wananchi pamoja na mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi Halt ambao walithibitisha mtuhumiwa kukutwa na risasi hizo 12 zikiwa katika mfuko wa Rambo nyeusi katika nyumba aliyokuwa akiishi hapo kambuzi.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA