WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO WANAKABILIWA NA KITISHO CHA HAKI ZAO KUTOPATIWA KIPAUMBELE

Na.Issack Gerald

Imebainika watu wenye ulemavu Mkoani Katavi bado wanakabiliwa na kitisho cha haki zao za msingi kutopati wa kipaumbele na hivyo kuchochea unyanyapaa kuendelea kuwa mkubwa dhidi ya makundi hayo.

Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa kupinga ukatiri dhidi ya watu wenye ulemavu na kujadili namna matatizo ya watu wenye ulemavu yanashghulikiwa.

Kwa upande wa mratibu wa mradi wa elimu jumuishi Mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronica Mavanza pamoja na mratibu wa mradi huo Mkoani Katavi Raphael Fortunatus,wameahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakumba watu wenye ulemavu katika Mkoa ya Rukwa na Katavi.

Mkurugenzi wa Shirika la International Aid Service(IAS) kutoka nchini Denmark Bw.Torben Madsen mara baada ya kikao cha leo,amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu hasa katika sekta ya elimu.

Makundi ya Mtandao wa wazazi wenye ulemavu Wilayani Mpanda,Vyama vya watu wenye ulemavu na viongozi wa dini wameshirikishwa katika kikao hichio.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA