WANAFUNZI WATAKA AHADI YA ELIMU BURE ITEKELEZWE

Na.Issack Gerald-Mpanda
BAADHI ya wanafunzi wa darasa la saba wanaohitimu elimu ya msingi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamewataka wagombea wa nafasi mbalimbali  za uongozi watakaoshinda katika uchaguzi wa mwezi Oktoba kuhakikisha wanatekeleza ahadi ya kutoa elimu bure.
Kauli hiyo imetolewa leo na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi zilizopo katika Manispaa ya Mpanda ikiwemo shule ya Msingi Kashato.
Wakati huo huo Msimamizi mkuu wa mitihani katika shule ya Msingi Kashato mwalimu Sekela Mayeji, amesema Jumla ya wanafunzi 108 wamefanya mtihani katika hali ya  utulivu.

Katika mtihani huo Jumla ya wanafunzi wapatao laki saba kote nchini wanatarajia kumaliza mitihani ya kuhitimu darasa la saba leo. 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA