WALIMU 16 WAFUTWA KAZINI


JUMLA ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya kubainika wametenda makosa mbalimbali.
Hatua hiyo imethibitishwa jana na Katibu wa tume ya utumishi wa walimu TSC wilayani humo  Richard Katyega mbele ya kamishina wa tume ya Utumishi wa walimu Taifa,Samwel Koroso ambapo alisema  kuwa katika kipindi hicho  walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya kubainika kuwa na vyeti bandia.
Alisema katika mwaka wa fedha wa 2016,2017 na 2018  tume hiyo imesikiliza mashauri hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata mmoja na kutenda haki kwa mujibu wa sheria.
Katyega alisema tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua ikiwahamasisha walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze kukumbana na adhabu mbalimbali ikiwemo kufukuzwa kazi kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake kamishna wa tume ya TSC Samwel Koroso alionyesha kusikitishwa na vitendo vya  uvunjifu wa maadili kwa waalimu hali inaoyopelekea  kufukuzwa kazi na kuwa wao kama tume ya maadili kwa walimu wataendelea kuwachukulia hatua Walimu wote ambao watakwenda kinyume na maadili ya ualimu.
Aliwataka walimu kwenda sambamba na misingi ya sheria ya utumishi kwa walimu kama inavyowataka na kuongeza kuwa walimu wilayani humo hawana budi kuzipitia sheria za utumishi wa walimu ili waishi kwa kufuata sheria hizo kama zinavyoagiza.
Maofisa  kutoka ofisi ya ya kamishina wa tume hiyo nao walikutoa mada mbalimbali zilizolenga kuwapatia elimu Walimu na kuwakumbusha sheria za utumishi wa walimu,huku walimu kwa upande wao walipata fursa ya kueleza changamoto zinazo wakabili  na zilipatiwa majibu kutokana na maswali waliyokuwa nayo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA