ZITTO ATAKA TAMISEMI IMTAFUTE MWENYEKITI WA HALAMSHAURI ALIYETOWEKA
Mbunge
wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo),Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi
kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Kakonko, Simon Kangue.

“Habari
zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo,sisi watu wa
Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,”
amesema.
Zitto
amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na
kukutana na ofisa usalama wa wilaya.
Amesema
tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta
kufanyika.
“Familia
imechukua hatua mbalimbali,imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye
vikao,hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,”alisema Zitto.
Comments