WAKAZI WAOMBA TOZO ZA ZIMAMOTO ZISITISHWE MPAKA WAPATE UMEME NA BARABARA IMARA,KAMANDA AJIBU.

Na.Issack Gerald
Wakazi wa Kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wameliomba jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi,kutowatoza tozo za tahadhari ya majanga mpaka wapatiwe huduma ya umeme na kuboreshewa miundombinu ya barabara.
Wametoa ombi hilo na kusema kwa sasa hawaoni umuhimu wa kutozwa tozo hiyo,wakati nyumba zao hazina umeme na barabara hazipitiki kiurahisi.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi hilo Mkoani Katavi Abdallah Maundu amesema,tozo wanazotoza ni kwa mjibu wa sheria ya nchi na wanatoa huduma katika majanga ya moto pia katika ajali.
Maeneo mengi ya Mkoa wa Katavi yana tatizo la miundombinu ya barabara isiyopitika hasa msimu wa masika,jambo ambalo jeshi la zimamoto na uokoaji linatakiwa kujipanga namna litakavyotoa huduma kwa wakazi waishio katika maeneo ya miundombinu mibovu ya barabara.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA