MLIPUKO WA KIPINDUPINDU WILAYANI TANGANYIKA MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando,amethibitisha kipindupindu kuingia katika wilaya hiyo.
Muhando amesema mpaka kufikia jana Desemba 3,2017 wagonjwa 3 wameripotiwa kulazwa katika zahanati ya Isengule kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo.
Aidha Muhando amesema wanaendelea kufuatilia maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tanganyika kwa kuwa inasemekana tatizo lipo maeneo mengi ya Wilaya ya Tanganyika.
Kufuatia hatua hiyo,Mkuu wa Wilaya amewataka wakazi wa Wilaya ya Tanganyika kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo ikiwemo kuhakikisha kunakuwepo na usafi wa mazingira.
Kwa kawaida binadamu hupata ugonjwa wa kipindupindu kwa kula kinyesi kibichi cha binadamu ambacho kwa kiasi kikubwa husambazwa na nzi.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA