RC RUKWA : VIONGOZI WA DINI MUOMBEENI RAIS MAUGUFULI NA WATENDAJI WAKE

Na.Issack Gerald
MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaomba viongozi wa dini mkoani humo kuendelea kumuombea rais John Magufuli pamoja na watendaji wengine  wa serikali ili waongoze wananchi kwa kuzingatia misingi ya haki usawa na kuwaletea maendeleo  endelevu.
Wanagabo ametoa ombi hilo maalumu huo wakati akichangia shilingi milioni moja kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kusaidia ujenzi wa kituo cha afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa katika Tarafa ya Kirando Kata ya Kirando Wilayani Nkasi mkoani humo.
Amesema rais na watendaji wa serikali ya awamu ya tano wanahitaji kuombewa daima kwani kufanya kazi ya kuwaongoza wananchi ni jukumu zito linalohitaji msaada wa Mwenyezi Mungu.
Waka huo huo amesema taasisi za kidini kwa muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia linasaidia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala inayoongoza serikali.
Ametoa mchango huo kwa lengo la kuzindua harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya katika siku ya maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Kabwe Kata ya Kabwe wilayani Nkasi ambapo alikuwa rasmi katika sherehe hizo.
Kwa upande wake katibu wa Bakwata mkoani Rukwa Mohammed Khatibu amesema Baraza hilo linahitaji kiasi cha shilingi 6,910,000 ili kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya ambacho kipo katika hatua ya upauaji.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA