CWT MKOANI KATAVI WAMEANZA KUCHARUKA KUHUSU MADAI YA WALIMU

Na.Issack Gerald
Chama cha Walimu mkoa wa katavi CWT kinakusudia kuchukua hatua zaidi kutokana na fedha za walimu  manispaa ya Mpanda za makato katika mfuko wa Jamii PSPF kwa  2008 kutofikishwa.
Hatua hiyo imebainishwa na Katibu wa chama cha walimu mkoani Katavi Hamisi Chinahova ambapo amesema suala hilo halijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa.
Katika hatua nyingine amelitaja suala la kukithiri kwa madai mbali mbali ya walimu kuwa kikwazo katika utendaji kazi ikiwemo kufikia Malengo ya kitaifa.
Mwaka 2015 yaliibuka madai haya na kupelekea baadhi ya walimu kufanya maandamano ya amani mpaka ofisi ya mkuu wa mkoa ili kushinikiza malipo ya madeni zikiwemo stahiki mbali mbali.
Mwezi uliopita Rais Magufuli alisema madai yote ya watumishi wa umma yangelipwa mwezi uliopita.

 Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA