WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAMETAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI KUELEKEA MWISHONI MWA MWAKA.

Na.Issack Gerald
Katika kuelekea siku kuu za mwishoni  mwa mwaka Waendesha vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria za usalama bararani.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Katavi Bw.Nassoro Alfi ambapo amesema madereva wanatakiwa kuwa makini ikiwa pamoja na kufuata alama za barabarani.
Aidha mwenyekiti huyo ameuomba uongozi wa manispaa ya Mpanda kuweka vibao vya alama za usalama barabarani katika manispaa ili kupunguza ajali barabarani.
Katika hatua nyingine Bw. Alfi amesema Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani mwaka 2017  kimkoa wa katavi yanatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 17 hadi 20 mwezi.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA