WAKULIMA WAMESHAURIWA KUWEKA KIPAUMBELE KILIMO CHA MAZAO YA CHAKULA

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Wakulima wametakiwa kuyapa kipaumbele mazao ya chakula katika msimu wa huu wa kilimo ili kuwa na uhakika wa chakula
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi Lilian.
Matinga wakati akihutubia mkutano wa ufunguzi wa msimu wa kilimo ulifanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi kakese
Bi matinga amesema kuwa ili kuweza kupiga vita njaa wananchi wote hawana budi kulima kwa nguvu zao zote ili kuhakikishia akiba ya kutosha ya chakula mwisho wa msimu
Katika hatua nyingine Bi Matinga amewataka maafisa ugani kuwa na mashamba darasa ili yawasidie wakulima kulima kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wameishukuru hatua ya manispaakuzindua mradi huo katika kijiji chao na kuwasogezea huduma za pembejeo za kilimo katika maeneo yao.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA