WAKAZI KITONGOJI CHA SITUBWIKE WADAIWA KUKAIDI KUONDOKA HIFADHINI

Na.Issack Gerald-Katavi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga,amewataka wananchi wa Kitongoji cha Situbwike waliovamia Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kuanzisha shughuli za kibinadamu kinyume cha sheria waondoke kwa hiari ndani ya wiki mbili zijazo kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
Naibu Waziri Hasunga amesema hayo baada ya kutembelea kitongoji hicho chenye zaidi ya kaya 82 ndani ya hifadhi hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutatua migogoro katika maeneo ya hifadhi nchini.
Nao baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho wamekiri kuwa wapo ndani ya hifadhi na kwamba walipewa eneo hilo bila ya wao kujua na uongozi wa kijiji cha Stalike ambao kwa sasa haupo madarakani.
Serikali ya Wilaya ilitoa notisi ya siku 30 kwa wananchi hao kuondoka katika eneo hilo jambo ambalo halijatekelezwa huku taarifa zikieleza kuwa baadhi yao wamekaidi kuondoka kwa madai kuwa mpaka waone polisi ndio watafungasha virago vyao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Waziri huyo alikuwa mkoani Katavi juzi kwa ajili ya ziara

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA