MADIWANI MANISPAA YA MPANDA WAMETOA TAMKO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UONGOZI WAKE

Na.Issack Gerald-Katavi
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa Mpanda mkoani  Katavi  wamempongeza rais John Magufuli kwa ujasiri aliouonesha wa kulinda  rasilimali za nchi  hasa  katika suala la madini.
Pongezi hizo zilitolewa jana kupitia waandishi wa habari ambapo Meya wa Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo alizungumza niaba ya madiwani hao.
Aidha Mbogo alisema wanawalaani vikali baadhi ya watu ambao wanaobeza jitihada zinazofanywa  na rais  za kulinda rasilimali zetu za  nchi na hasa madini  kwa  ajili ya  manufaa ya Watanzania  wote.
Alisema madiwani wa  Manispaa ya Mpanda wanaamini mapato hayo yatakayopatikana  yataongezeka  Serikalini na halmashauri zote zitaongeza uwezo wa kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake diwani wa Kata ya makanyagio Haidari  Sumry aliomba jitihada za rais zisiishie kwenye madini tu bali nguvu iongezeke kwenye   maeneo   mengine   iliuchumi wa  nchi ukue na kuongezeka zaidi ya hivi sasa. 
Alisema endapo rasilimali za nchi zitasimamiwa vizuri halmashauri zitanufaika na mapato yataongezeka Serikalini kwani hata huduma  kwenye halmashauri zitaboreshwa zaidi.
Naye diwani wa viti maalumu katika halmashauri hiyo Getruda  Kabinda alisema watu waliokuwa wakinufaika peke yao na rasilimali za nchi ndio wanaobeza na kupinga jitihada zinazofanywa na rais kwa manufaa ya watanzania wengi katika kulinda  rasilimali za nchi.
Alimuomba rais Magufuli kukaza uzi kwani watanzania wanyonge wanatambua anachokifanya na kamwe asikatishwe tamaa na wasaliti wachache kwa maslahi yao,kwani hatua anazochukua japo siku moja atakufa lakini atabaki anaishi katika mioyo ya wanyonge Kama baba wa taifa  mwalimu Julius Nyerere.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA