TEHERAN
Afisa wa ngazi ya juu katika sekta ya elimu nchini Iran ametaka lugha ya Kiingereza isiendelee kufundishwa katika shule za msingi nchini humo.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni ya taifa ya Iran jana Jumapili, afisa huyo, Mehdi Navid-Adham ambaye ni kiongozi wa Baraza la Elimu ya Juu amesema Kiingereza ni mkondo wa uvamizi wa kitamaduni wa nchi za Magharibi.

Mwaka 2016 Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitoa mapendekezo kama hayo, baada ya kuarifiwa kuwa baadhi ya shule za chekechea zilikuwa zikiwafundisha watoto kwa lugha ya Kiingereza.


Tangazo hilo limekuja wiki moja baada ya maandamano dhidi ya serikali kulalamikia hali ngumu ya uchumi, maandamano ambayo Khamenei alisema yaliratibiwa kutoka nje ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA