KIDATO CHA KWANZA WARIPOTI KWA KASI KATIKA SHULE MBALIMBALI MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha kwanza ambao wameripoti katika shule mbalimbali za sekondari Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamesema wamejiandaa kusoma kwa bidi ili kuwa na ufaulu mzuri kitaaluma.
Miongoni mwa Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mwangaza wamesema wamejiwekea mikakati yao kuhakikisha wanafaulu kwa kiwango kinachotakiwa kitaaluma ambapo wanafunzi hao wanatoka katika shule mbalimbali za msingi zikiwemo Kawanzige,Kakese,Mwangaza,uhuru, Kashato,Kashaulili na Katavi.
Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Mwangaza iliyopo Manispaa ya Mpanda Simon Lubange amesema,mpaka sasa wanafunzi karibu ya 200 kati ya 260 wanaotakiwa kuripoti katika shule hiyo wameripoti ili kuanza masomo.
Nao baadhi ya wazazi ambao wamewapeleka shule watoto wao wamesema ni wakati wa kila mzazi kutambua umuhimu wa elimu kwa kila mtoto kwa maisha ya baadaye.
Hata hivyo kwa mjibu wa takwimu iliyotolewa mwaka uliopita na Afisa elimu Mkoani Katavi Ernesti Hinju inaonesha zaidi ya wanafunzi 9000 wanalizimika kutojiunga mapema na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA