WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA,DC ATOA KAULI

Na.Issack Gerald
Mkuu wa wilaya ya mpanda Liliani Charles Matinga ameamuru masoko yote kufunguliwa  baada ya wafanyabiashara kufanya  mgomo kutokana na ongezeko la tozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kodi.
Amri hiyo ameitoa leo asubuhi wakati akiwa soko kuu  ambapo wafanyabiashara waliogoma  kufungua biashara zao huku akisema kwa anayeshindwa arudishe  chumba cha biashara.
Amesema wamekaa na wafanyabiashara kwa ajili ya kupanga ongezeko hilo ambapo hapo awali halimashauri ilipanga laki moja na baada ya hapo  ikapungua hadi elfu sitini.
Awali wafanya biashara hao wamesema walishindwa kumudu kodi iliyokuwepo ya shilingi 15000 ambapo wamesema serikali kuwatoza shilingi 60000 ni kuendelea kuwakandamiza.
Masoko amabyo wafanyabiashara wamefunga biashara zao ni Soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe lenye zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 500 hii ikiwa ni kwa mjibu wa baadhi ya wafanyabiashara.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA