RAIS AMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI,AMTENGUA KAMISHNA WA MADINI NA KUTEUA MWINGINE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini na kuiagiza Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha kanuni za sheria mpya ya madini namba 7 ya mwaka 2017 inasainiwa ifikapo Ijumaa tarehe 12 Januari 2018.
Mh.Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya Mhe.Biteko kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na ameelezea kutoridhishwa kwake na namna viongozi na watendaji wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu yao polepole na bila kujali maslahi ya nchi.
Amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kushirikiana na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi wanaohusika katika Wizara ya Madini kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa.
Pamoja na maagizo hayo Mh.Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka na amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini.
Kabla ya uteuzi huu Prof.Shukrani Elisha Manya alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Jiolojia.
Mh.Rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote atayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA