DC ACHARUKA WANANCHI KUTAPELIWA FEDHA ZA MASHINE ZA EFDs


SERIKALI mkoani Katavi imetoa siku 14 kwa makampuni na wafanyabiashara waliochukua fedha kwa ajili ya kuwauzia mashine za EFDs wafanyabishara na mpaka sasa hawajui hatma ya fedha zao.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lllian  Matinga alitoa siku hizo jana  katika kikao maalumu cha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa mkoa huo akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja jenerali  Mstaafu  Raphae Muhuga.
Alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa makampuni yaliyokusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara na kuahidi kuwapelekea mashine za EFDs lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo.

Matinga alisema kutokana na kuwa wafanyabiashara hao hawajui hatma ya fedha zao na mpaka sasa hawajapata mashine hizo hivyo ameamua kutoa siku hizo warudishiwe fedha zao vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.
Awali katika kikao hicho mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mkoa huo Hasanaal  Dalla alimwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa wafanyabiashara wa mkoa huo wametapeliwa na makampuni ambapo yamechukua fedha zao kwa ahadi kuwa watawaletea mashine za EFDs lakini imekuwa ni tofauti.
Alisema imepita muda mrefu mpaka hivi sasa ambapo fedha za wafanyabiashara zimechukuliwa na hawajui hatma yao ni nini hivyo alimuomba mkuu huyo wa wilaya awasaidie.
Mwenyekiti huyo alisema baadhi ya wafanyabiashara wanaonekana hawatii agizo la serikali la kuwataka watumie mashine hizo lakini ukweli ni kwamba walikwisha lipa fedha ili wapate mashine hizo lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya huyo mwaka jana alitoa agizo kama hilo kwa makampuni na wafanyabiasahara hao lakini haijajulikana kama agizo lake lilitekelezwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA