MPANDA RADIO YAONGOZA WANANCHI KATAVI KUSHEREHEKEA VALENTINE DAY KWA KUCHANGIA DAMU SALAMA

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh.Salehe Mbwana Muhando,amekipongeza kituo cha matangazo cha Mpanda Radio kwa kuadhimisha siku ya wapendanao kwa kuwaunganisha Watanzania kwa kuchangia damu salama ili kunusuru wagonjwa.
Akizindua kampeni hiyo ya uchangiaji damu salama iliyoandaliwa na kuratibiwa na Mpanda Radio Muhando ambaye amemwakilisha Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,amewataka Watanzania kuwa na moyo wa kujitolea katika mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo uchangiaji damu salama kwa ajili ya watu wenye uhitaji.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mpanda Radio Bi.Salome Mchawa,amesema Mpanda Radio kama radio ya kijamii itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kujali mahitaji ya jamii huku akiwashukuru na kupongeza watanzania kwa kuunga mkono kampeni ya uchangiaji damu salama iliyoanzishwa na Mpanda Radio kama kushrehekea siku ya wapendanao’’Valentine Day’’.
Kituo cha Matangazo cha Mpanda Radio Fm kilichoanzishwa mwaka 2013 na kuzinduliwa na mwenge wa uhuru Julai 17,2013 kimeendesha zoezi la kuchangia damu salama huku kauli mbiyu ikisema‘’Changia Damu salama Okoa Maisha’’.
Kampeni hii iliyoanza kuwahamasisha wananchi tangu mwezi uliopita imewahusha viongozi wa kiserikali,vyama vya siasa, mashirika ya kiserikali na kiraia pamoja Wanakatavi .
Siku ya wapendanao maarufu ‘’Valentine Day’’ ni siku ya Kumkumbuka Padre aliyeitwa Mtakatifu Valentine aliyeuwawa na warumi akipinga watu kufanya ngono bila kuoa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA