AUAWA KWA KUKANYAGWA NA TEMBO


MWANAMKE  aliyefahamika kwa jina la Maria Sekaye(60) mkazi wa kijijii cha Ilambila wilayani Kalambo  Mkoani Rukwa ameuawa baada ya kukanyagwa na tembo.
Tembo hao wanaelezwa kuwa walikuwa njiani wakitokea katika pori la akiba la Lwafu mkoani Rukwa kuelekea katika nchi jirani ya Zambia.
Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya Mkowe Alfred Mpandasharo alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 za asubuhi wakati mwanamke huyo akiwa ametoka kutembelea shamba lake lililokuwa limevamiwa na mazao kuliwa na tembo hao.

Alisema Maria akiwa njiani kurejea kijijini ghafla alikutana na kundi kubwa la tembo waliokuwa na hasira wakiwa wamechokozwa na vijana wa kijiji hicho kutokana na kuwafukuza kwa makelele ili waondoke kijijini hapo waache kula mazao katika mashamba yao na ndipo kundi la tembo lilimvamia na kuanguka chini ambapo alikanyagwa na kufa papo hapo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura aliwaonya wananchi wanaowafukuza hovyo tembo hao waache tabia hiyo kwani ni hatari kwa usalama wao wasubiri watendaji wa maliasili ambao watafika kwa ajili ya kuwafukuza kijijini hapo.
Bi.Binyura alisema  kwa kawaida katika vijiji vya  Sundu,Mkowe Ilambila na Katete huwa ni mapito ya tembo ambapo mara kwa mara wamekuwa wakipita kuelekea nchini Zambia na baadaye kurejea tena nchini katika pori la akiba la Lwafu.
Alisema ni vizuri wananchi wakaacha kufanya kilimo na kujenga makazi katika mapito ya tembo hao kwa kuwa kawaida huwa hawaachi kupita hata kama itachukua miaka mingi lakini kunasiku watarejea na kupita tena hivyo ni hatari kwao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA