RAIS MAGUFULI AMTEUA MNADHIMU WA JWTZ APANDISHA VYEO MABRIGEDIA 10 KUWA MAJENERALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Rais wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli
Pamoja na uteuzi huo,Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.
Kwa mjibu wa taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu ya Rais,Gerson Msigwa Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.
Aidha,Mhe.Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;
1.                         Brig Jen. J.G. Kingu
2.                        Brig Jen. M.S. Busungu
3.                        Brig Jen. R.R. Mrangira
4.                       Brig Jen. B.K. Masanja
5.                        Brig Jen. G.T. Msongole
6.                       Brig Jen. A.F. Kapinga
7.                        Brig Jen. K.P. Njelekela
8.                       Brig Jen. A.S. Bahati
9.                       Brig Jen. M.E. Mkingule
10.                     Brig Jen. S.S. Makona
Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye huku Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akitarajiwa kuapishwa kesho 15 Februari 15 kuanzia saa saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA