RAIS MAGUFULI APUZILIA MBALI WARAKA WA MAASKOFU


Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameupuuzilia mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hauna msingi wowote ule.
Rais Magufuli amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kuongozea ndege jijini Dar es Salaam.
Majibu yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri,viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine akisema wanaendelea kutimiza vizuri majukumu yao.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kujibu moja kwa moja waraka uliotolewa na maaskofu wa kanisa la Kilutheri nchini Tanzania siku chache zilizopita ambao pamoja na mambo mengine ulionya juu ya mwenendo wa demokrasia nchini Tanzania.
Katika waraka wa ujumbe wa Pasaka uliosomwa katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii,baraza hilo liliorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
Walitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni utesaji,kupotea kwa watu,mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa,mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi,vitisho, ubambikiziaji wa kesi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
Serikali ya Tanzania hivi karibuni kupitia kwa Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari,Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ilikuwa imesema wakati waraka ukitoka haikuona cha kujibu zaidi ya kuwatakia tu waumini kheri ya Pasaka.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA