RAIS MAGUFULI ATOA AGIZO ZITO KWA KAMISHINA WA UHAMIAJI NCHINI

Rais John Magufuli ameitaka Idara ya Uhamiaji kuhakikisha inapambana na wahamiaji haramu pasipo kumwogopa mtu.
Amemwagiza Kamishna wa Uhamiaji,Dk Anna Makakala kuwachukulia hatua kali watumishi wake watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli
Dk.Magufuli akizungumza leo akizindua hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam,amesema utambuzi wa wananchi wanaoishi bila vibali na wenye vibali vilivyoisha ni muhimu.
Amesema uhamiaji ina jukumu kubwa katika kutekeleza hayo.
Amesema awali Uhamiaji iligubikwa na matatizo yakiwamo ya utoaji hovyo wa vibali vya uraia, hata kwa watu ambao walikuwa hawana sifa.
Dk Magufuli amesema hiyo ndiyo sababu iliyofanya akamteua Dk Makakala kuwa Kamishna. "Wanawake ni waaminifu sana na ameanza kutatua matatizo haya."
Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Wengine ni marais wastaafu Amani Abeid Karume na Ali Hassan Mwinyi,Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Ali Iddi.
Pia viongozi wa Serikali,Bunge,Baraza la Wawakilishi,wa dini,wanasiasa,na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA