MKOA WA KATAVI KUUNGANISHWA NA GRID YA TAIFA

WAZIRI wa Nishati Dr.Merdard Kareman   amesema miaka miwili ijayo shirika la umeme Tanesco mkoani Katavi litakuwa limeunganisha Mkoa wa Katavi katika gridi ya taifa.

Waziri Kareman  ametoa kauli hiyo wakati akikagua mradi wa mashine za kuzalisha umeme katika mji wa Inyonga wilayani.

Amesema mpaka kufikia mwaka 2019 maeneo mengi hasa vijijini yatakuwa yameunganishwa na umeme ili kuongeza kasi ya uchumi wa viwanda mkoani Katavi.

Kwa sasa Mkoa wa Katavi unatumia jenereta kuzalisha umeme unaotumika ktika wilaya za Mpanda,Mlele na Katavi ambapo wakazi wengi wamekuwa wakilalamikia tatizo la umeme jenereta linapokuwa na tatizo.

Waziri Kareman  ambaye alifanya ziara Mkoani Katavi akitokea Mkoani Kigoma aliendelea na ziara Mkoani Rukwa.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA