MADIWANI WATATU CHADEMA WASIMAMISHWA

Madiwani watatu wa CHADEMA halmashauri ya Mji wa Njombe wametolewa nje ya kikao cha baraza la madiwani na kusimamishwa kuhudhuria vikao 3 kutokana na kujadili mkataba wa halmashauri na kampuni iliyowekwa kukusanya ushuru ambayo inawanyanyasa wananchi.
Madiwani hao ni pamoja na George Sanga diwani Kata Ramadhani,Sigrada Mligo,diwani viti maalum,Legnard Danda diwani kata Ihungilo.
Madiwani hao walitolewa kwenye mkutano na kusimamishwa kuhudhuria vikao vitatu baada ya kuhoji mkataba wa halmashauri na kampuni ya Ihagara inayo kusanya ushuru mjini Njombe ambayo inadaiwa kuwanyanyasa wananchi. 
Awali Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Edwin Mwanzinga alipiga marufuku kujadili suala hilo kwa madai kuwa baraza halina mkataba huo na hakuna palipo andikwa jina la kampuni hiyo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA