RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA MZEE MAJUTO HOSPITALI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe,Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa.
Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.
Pamoja na hayo,Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ;“sisi wazee tunafarijika sasa hivi,viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara.
Kwa upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt.John Magufuli.
Chanzo:Bongo5.com

Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA