TPA MKOANI RUKWA IMETOA MSAA WA SHUKA 1245 KATIKA IDARA YA AFYA

MAMLAKA ya bandari nchini(TPA) imetoa msaada wa mashuka 1245 yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa halmashauri ya wailaya ya Nkasi kwaajili ya idara ya afya wilayani humo.
Mkurugenzi wa bandari nchini Desderius Kakoko alisema kuwa msaada huo wanatoa katika halmashauri ambazo zina bandari kote nchini ikiwa ni sehemu ya kutoa ahasante wa halmashauri hizo.
Alisema kuwa mamala ya bandari nchini inachangia nusu ya makusanyo ya taifa kwa mwezi ambayo ni shilingi bilioni Mia 5.5 ambapo inatumika katika matumizi ya serikali. 
Kakoko alisema kuwa kutokana na wilaya ya Nkasi kuwa na mahitaji katika idara ya afya mamlaka hiyo imeamua kuchangia mashuka ikiwa ni katika jitihada za kupunguza matatizo kwa wananchi. 
Alisema nchi ya tanzania inapakana na nchi nane ambazo hazina bandari nazinategemea bandari zilizopo hapa nchini hivyo basi nifursa nzuri ya kuhakikisha kuwa uchumi unakua nakuongeza pato la taifa.
Akishukuru kwa msaada huo mbunge jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy alisema kuwa msaada huo umekuja katika wakati muafaka kwani sekta ya afya wilayani humo bado inamahitaji makubwa. 
Alisema kuwa msaada huo sio mara ya kwanza kwa wilaya hiyo kwani mamlaka ya bandari iliwahi kutoa msaada wa shilingi  milioni 40 taslimu kwaajili ya kusaidia sekta ya elimu na afya. 
Hata hivyo aliisihi mamlaka ya bandari nchini kuhakikisha inakuamakini na upande wa Zanzibar kwani kuna bandari bubu nyingi zinazoikosesha serikali mapato. 
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5tanzania Limited


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA