WAZIRI LUKUVI MKOANI RUKWA NA MASUAL AYA MIGOGORO YA ARDHI

Uzembe na utendaji kazi wa kimazoea kwa baadhi ya watendaji wa serikali wakati wa ubinafsishaji wa shamba la Mlonje Dafco lenye ukubwa wa hekta 10,000 na kumpa mwekezaji Tasisiya Efatha Ministry umewagharimu wananchi na kuibua migogoro ya mara kwa mara baina ya mwekezaji huyo na vijiji jirani vinavyozunguka shamba hilo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi amesema hayo leo mjini Sumbawanga wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali ngazi ya mkoa, na halmashauri za wilaya ya Sumbawanga mjini na vijijini, wakiwemo wabunge wa majimbo ya Kwela na Sumbawanga mjini.
Uzembe huo umesababisha serikali kukirimakosa katika zoezi zima la kubinafsisha Shamba hilo hali iliyosababisha mgogoro huo kushindwa kutatuliwa kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa RDC mjini hapa, Waziri Lukuvi alisema kwamba mwekezaji huyo anapaswa kuachwa ili kuendelea na shughuli zake kwa kuwa shamba hilo alipewa kihalali kwani waliofanya makosa wakati wakibinafsisha kwa mwekezaji ni watendaji wa serikali ambao walifanya hivyo pasipo kufuata maelekezo ya serikali.
Alisema njia pekee ya kutatua tatizo la baadhi ya vijiji kikiwemo cha sikaungu ambacho wananchi wake wanalalamika kukosa radhi kwa ajili ya shughuli za kilimo ni wizara kufanya mazungumzo na mmliki wa shamba hilo na kuomba atoe ardhi kidogo kwa kijiji hicho.
Alisema iwapo wataafikiana  itawalazimu wizara kupitia upya michora ya hati yake na kugawa sehemu ya ardhi hiyo kwa kijiji hicho hali ambayo itafanya na yeye aweze kufanya shughuli za uwekezaji pasipo kuingilia na mtu yeyeto hivyo uwekezaji wake kuleta tija tofauti na ilivyo sasa ambapo amekuwa akikabiliana na changamoto za migogoro kadhaa.
Mgogoro wa Shamba la Dafco Malonje umedumu kwa zaidi ya miaka tisa sasa, ambapo iliuzwa kwa mwekezaji huyo mwaka 2008 na uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kwa maelekezo ya uongozi wa mkoa wa Rukwa, kwa bei ya milioni Sh 600,000,000.
Awali,Mbunge wa Sumbawanga mjini,Aeshi Hilaly akizungumza katika kikao hicho aliomba serikali itakapofanya mazungumzo na mwekezaji huyo kuhusu kupitia upya mipaka iweze kumshawishi ili atoe ardhi kwa vijiji vyote 24 vinavyozunguka shamba hilo hali ambayo itasaidia kumaliza migogoro ya ardhi.
Mkuu wa mkoa huo, Zelothe Steven aliwataka wananchi wa vijiji vinavyozunguka shamba hilo kuelewa kwamba serikali ipo kwa ajili ya kutatua matatizo yao hivo sasa wanapaswa kuwa watulivu na kujitojiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na watachukuliwa hatua stahiki ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA