WATATU KATAVI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI


Na.Issack Gerald-Mpanda
Jeshi la polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu watatu kutokana na kukamatwa na nyara za serikali ambazo wamezipata kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Leonard Mbegele(38) mkazi wa Migazini na Anastazia Bernad(38) mkazi wa kichangani ambao walikamatwa mnamo tarehe 22.12.2015 majira ya saa 13:00 maeneo ya Mikocheni Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mkoani Katavi wakiwa na nyama ya Kongoni kilo moja.
Kamanda amesema kuwa Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema lilifanya upekuzi nyumbani kwa Anastazia Bernard ambapo nyama hiyo ilikutwa ikiwa imewekwa kwenye Hotpot iliyokuwa ndani ya kabati.
Katika upelelezi wa awali wa tukio hiliAanastazia alidai kuwa nyama hiyo ni ya Malack Jonas ambapo hata hivyo Jonas naye aliikana nyama hiyo.
Mpaka sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika.
Wakati huo huo Leornard Mbegele (38) Mkazi wa migazini Kata ya Nsemulwa, Tarafa ya Kashaulili, Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mnamo tarehe 22.12.2015 majira ya saa 14:00  anashikiliwa na alikamatwa akiwa na nyama ya Kongoni kilo 15.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishewa mahakamani upelelezi utakapokamilika.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA