MAUAJI KATAVI


Na.Issack Gerald- Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  KAZIMIRI MASUMBUKO(49) MKAZI NA MKULIMA WA MISANGA aliuawa kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali sehemu za mgongoni, mkononi, mkono wa kushoto na kidevuni na watu wasiofahamika
                                              
Kamanda wa polisi Katavi-Dhahiri Kidavashari
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kmanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili tarehe 20.12.2015 majira ya saa katika kitongoji cha Misanga Kata na Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa, siku ya tukio hilo,watuhumiwa wasiofahamika kwa sura wala idadi yao walifika nyumbani kwa marehemu wakakuvunja mlango na kuingia moja kwa moja hadi chumbani kwa marehemu na kumpeleka sebureni kwake kisha kutekeleza mauaji hayo na kutokomea kusikojulikana .
Mpaka sasa chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika. Hata hivyo Upelelezi wa shauri hili unaendelea kwa kufanya msako kwa kushirikiana na wakazi wa kata ya Misanga kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa agizo kwa wananchi kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mikononi dhidi ya migogoro ya kijamii miongoni mwao, badala yake wajenge tabia ya kuheshimu na kutumia mamlaka za kisheria katika kutafuta ufumbuzi.
Amesisitiza kuwa ataendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale watakaoendelea kubainika kukiuka maagizo hayo kutokana na visingizio mbalimbali
Endelea kufuatilia habari mbalimbali kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA