BUNGE NCHINI BURUNDI NA BALAZA LA SENATE NCHINI HUMO WAKUTANA KUJADILI HALI YA USALAMA BURUNDI


Na. Prosper Kwigize
Bujumbura, Burundi
Bunge la Jamhuri ya Burundi kwa pamoja na Baraza la SENATE leo wamekutana pamoja jijini Bujumbura kujadili hali ya usalama.

Katika kikao hicho kinachoongozwa na spika wa Bunge Bw. Pascal Nyabenda na Rais wa Senate Reverien Ndikuriyo, wanajadili kuhusu uvumi wa mauaji ya watusi.
Aidha agenda nyingine ni kujadili kuhusu uharali wa umoja wa Africa kutuma majeshi nchini humo pamoja na tabia ya washirika ya kimataifa kuandika ripoti za ongo kuhusu Burundi.
Katika kikao hicho kinachoendelea wabunge na wajumbe wa Baraza hilo wametaja kuwa uvumi wa mauaji ya kimbali ni wa uongo na kwamba unalenga kuharalisha hisia za baadhi ya mataifa kutaka kuiondoa serikali madalakani.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika kwa kukutanisha vyombo hivyo viwili unatarajia kutoa tamko la pamoja kulaani mataifa na makundi ya watu kuichafua Burundi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA