WAWILI MBARONI AKIWEMO KARANI WA CHUO CHA MAENDELEO MSAGINYA ,KWA SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI KATAVI


Na.Issack Gerald- Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo  ASHURA MSAGUSI(30) Karani wa chuo cha Maendeleo Msaginya Mkazi wa Kata ya Makanyagio na AISHA SUNGURA (28) Mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani kwa tuhuma za shambulio la mwili.
                                        
Kamanda wa Polisi Katavi-Dhahiri Kidavashari

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,Kmanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alisema kuwa tukio hilo limetokea Mnamo tarehe 17.12.2015 majira ya saa 5 asubuhi katika Mji wa Zamani Kata na Tarafa ya  Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Alimtaja aliyeshambuliwa kuwa ni JENEROZA ROBA(60 Mkazi wa Nsemulwa kwa Mkumbo ambapo alishambuliwa kwa kupingwa  ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa maumivu makali.
Kamanda Kidavashari alisema kuwa,siku ya tukio inasemekana kuwa mtuhumiwa ASHURA MSAGUSI alijifanya kupandisha mashetani na kuanza kumtaja Mtendewa JENEROZA ROBA kuwa anajihusisha na shughuli za uchawi ambazo zinaathiri familia zao. Kitendo hicho cha kupandisha mashetani kilimshawishi AISHA SUNGURA na hivyo kuungana na ASHURA MSAGUSI na kuanza kumshambulia mtendewa.

Watuhumiwa wote wawili ambao wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika.
Kufuati matukio ya kujichukulia sheria mkononi,Kamanda wa Polisi anatoa onyo wa watu wenye matukio hayo,ambapo amesema ataendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale watakaoendelea kubainika kukiuka maagizo hayo kutokana na visingizio mbalimbali.
Endelea kufuatilia habari mbalimbali kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA