AKIMBIA MKONO WA POLISI KUKWEPA KUKAMATWA KWA KOSA LA KUMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA


Na.Issack Gerald-Mpanda
Jeshi la polisi Mkoani Katavi linamtafuta mtu mmoja aliyekimbia akikwepa kukamatwa na polisi kutokana na kumiliki silaha aina ya gobore  kinyume na sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Malugumba Nzinza kukamatwa na silaha aina ya gobore ambayo imepatikana ikiwa imefichwa katika nyumba yake.
Kamanda kidavashari amesema mtu huyo alikamatwa,mnamo tarehe 12.12.2015 majira ya saa 12:00  katika kijiji cha Mpembe Kata na Tarafa ya  Mwese Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi.
Kamanda amesema kuwa katika tukio hilo,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori (TANAPA) walipata taarifa toka kwa raia wema kuwepo kwa mtu anayehisiwa kumiliki silaha kinyume na utaratibu.
Mpaka sasa mtuhumiwa bado hajakamatwa na misako mbalimbali inaendelea katika kuhakikisha mtuhumiwa anatiwa nguvuni na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA