MKE WA ZAMANI WA NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA-FAHAMU HISTORIA YAKE
WINNIE MANDELA ,mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake. Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936,na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990,Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw.Mandela. Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa:"Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwanzo wa mwaka na alifariki mapema leo Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake." Kwa mjibu wa shirika la habari la AFP Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama "ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi ambapo Winnie alikuwa na miaka 20 hivi akiwa katika siasa. Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na ...