MUFTI ZUBERI AFUNGA MKTANO MKUU WA BAKWATA AWAASA WAISLAMU KUBADILIKA
Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh
Abubakar Zuberi, amesema wakati umefika kwa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania,BAKWATA
kubadilika ili kuendesha shughuli zake kiuweledi na kuachana na kufanya kazi
kwa mazoea.
Mufti
Zuberi ametoa rai hiyo Mjini Dodoma leo wakati akifunga mkutano mkuu wa siku
mbili wa Bakwata.
Amesisitiza
haja ya baraza hilo kuelekeza nguvu zake katika kuwahudumia waumini wa dini ya
Kiislaam nchini ambapo amesema kufanya kazi katika mtindo huo kunalenga kuwaunganisha
Waislaam.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi wa Elimu wa Bakwata, Sheikh Ali Abdallah Ali amesema,mkutano
huo umewasilisha mapndekezo ya maazimio 32 kwa lengo la kulijenga baraza hilo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments