WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2018 ATAJA MIKOA INAYOONGOZA KWA UTORO SHULENI
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa amezindua mbio za
mwenge wa uhuru kwa mwaka 2018.
Akizindua
mbio hizo kitaifa Mkoani Geita,amewataka viongozi wa mikoa ya Tabora,Geita,Mtwara
na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za sekondari
wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni.
Akizungumzia
kuhusu utoro kwa shule za sekondari nchini,Waziri Mkuu amesema mkoa wa Tabora unaongoza
kwa utoro kwa kuwa na silimia 9.7,Geita asilimia 8.1,Mtwara asilimia 6.4 na
Shinyanga asilimia 6.3.
Kuhusu
utoro wa wanafunzi wa shule za Msingi nchini, Waziri Mkuu amesema mkoa
unaoongoza ni wa Rukwa kwa asilimia 3.2,Geita asilimia 3.1,Tabora asilimia 2.9,
Simiyu asilimia 2.0 na Singida asilimia1.9.
Aidha Waziri
Mkuu amesema dhamira ya Serikali ni kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali
wa maendeleo kuwekeza katika elimu na kuzalisha rasilimali watu yenye ujuzi na
stadi zitakazowezesha kuchochea mapinduzi ya viwanda ili nchi iwe ya uchumi wa
kati ifikapo 2025.
Awali,Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Bi.Jenista
Mhagama alisema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa takribani kilomita
103,440.7 kwa siku 195 katika mikoa yote 31 nchini na halmashauri za wilaya 195.
Aidha Bi.Mhagama
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 zinaongozwa na Bw.Charles Kabeho kutoka mkoa
wa Dar es Salaam akishirikiana na Bw.Issa Abasi Mohamed (Kusini Pemba),Bi.
Agusta Safari (Geita),Bw.Ipyana Mlilo (Tanga),Bw.Dominick Njunwa (Kigoma) na
Bi. Riziki Hassan Ali (Kusini Unguja).
Kwa upande
wake Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo - Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume alisema atahakikisha ujumbe wa Mwenge wa Uhuru
unawafikia wananchi wote pamoja na kupita katika miradi yote ya maendeleo
iliyopangwa.
Mbio
za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 zimezinduliwa katika uwanja wa Magogo mkoani
Geita ambapo Kaulimbiu ya mbio za mwenge
kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa
maisha,wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
Kwa mwaka uliopita mbio za mwenge wa
uhuru ambao ulianzishwa Desemba 9,1961 zilikuwa zimezinduliwa Mkoani Katavi
Aprili 2,2017 na Kuzimwa Okt 14,2017 visiwani Zanzibar.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments