MKE WA ZAMANI WA NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA-FAHAMU HISTORIA YAKE
WINNIE MANDELA,mke wa zamani wa Nelson Mandela,
ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki
dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
Winnie
alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936,na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela
- walitalikiana mapema miaka ya 1990,Winnie Madikizela Mandela kama
alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw.Mandela.
Msemaji
wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa:"Amefariki baada ya
kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa
mara tangu mwanzo wa mwaka na alifariki mapema leo Jumatatu adhuhuri akiwa
amezungukwa na familia na wapendwa wake."
Kwa
mjibu wa shirika la habari la AFP Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel
Desmond Tutu amemsifu kama "ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi
ambapo Winnie alikuwa na miaka 20 hivi akiwa katika siasa.
Alisomea
kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na
mwanasiasa.
Katika
kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya kuachiwa
huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa mwaka 1964,Bi
Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na pia kuendeleza kampeni
za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao waachiwe huru hasa mumewe.
Kutokana
na hayo Bi.Winnie Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford katika jimbo
lao la Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni mojawapo za kupambana
na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama the Soweto Uprising.
Bi.Mandela
mwaka 1988 alihusika makubwa kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kama
ilivyomtokea mumewe, Bi Winnie alifungwa gerezani,na hata kuwekwa katika
kizuizi cha pekee yake ambacho ni mojawapo ya vifungo vigumu zaidi gerezani
vinavyowaathiri wafungwa kisaikolojia.
Lakini
baada ya kuachiwa kwake mtindo wa mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi
ulianza kupata sifa mbaya hasa pale alipoonekana kuendekeza tabia ya kuwavisha
tairi shingoni wale waliolengwa kwa tuhuma za usaliti na kisha kuwachoma moto.
Walipatikana
kuhusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua kijana mmoja mwenye umri wa
miaka 14 aitwae Stompie Moeketsi -kwa tuhuma za kwamba alikuwa akitoa siri kwa
maadui zao.
Japo
Bi.Winnie Mandela aliepuka hukumu ya kifungo jela - baadaye tume ya ukweli na
maridhiano iliyoongozwa na askofu Desmond Tutu,iliyokuwa inachunguza ukweli
kuhusu matendo tata katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta
maridhiano,ilimpata Bi Mandela na hatia ya kutowajibika kisiasa wala kimaadili
wakati wa kitendo hicho.
Licha
ya misukosuko hiyo Bi.Mandela alibaki kuwa mtu muhimu sana katika siasa za
Afrika kusini na kuwa mwakilishi muhimu wa wanawake waliopambana kufa na kupona
dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendelezwa na Wazungu walio
wachache nchini humo.
Katika
siku za baada ya uhuru wa Afrika Kusini anakumbukwa zaidi kwa kuwa miongoni mwa
wachache katika uongozi wa ANC waliomuunga mkono aliyekuwa rais wa Afrika
Kusini Thabo mbeki katika kushtumu na kulaani vikali vitendo vya kuwashambulia
wahamiaji wa Kiafrika huko nchini Afrika Kusini.
Pia
amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha Economic Freedom
Fighters CHA Julius Malema,kilichojimegua kutoka ANC ambacho kilimkosoa vikali
rais aliyelazimika kung'atuka Jacob Zuma.
Historia
ya Bi.Winnie Madikizela Mandela,hadi kifo chake inabaki akikumbukwa zaidi kama
mama wa taifa la Afrika kusini aliyesimama kidete dhidi ya ubaguzi wa rangi
katika umri wake wote.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments