RAIS MAGUFULI APUZILIA MBALI WARAKA WA MAASKOFU
Rais
Magufuli amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada
za kuongozea ndege jijini Dar es Salaam.
Majibu
yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake,
mawaziri,viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine akisema
wanaendelea kutimiza vizuri majukumu yao.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli
kujibu moja kwa moja waraka uliotolewa na maaskofu wa kanisa la Kilutheri
nchini Tanzania siku chache zilizopita ambao pamoja na mambo mengine ulionya
juu ya mwenendo wa demokrasia nchini Tanzania.
Katika waraka wa ujumbe wa Pasaka
uliosomwa katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika
mitandao ya kijamii,baraza hilo liliorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja
kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
Walitaja
baadhi ya mambo hayo kuwa ni utesaji,kupotea kwa watu,mashambulizi ya silaha
dhidi ya viongozi wa kisiasa,mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi,vitisho, ubambikiziaji
wa kesi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
Serikali ya Tanzania hivi karibuni
kupitia kwa Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Habari,Maelezo na Msemaji
Mkuu wa Serikali ilikuwa imesema wakati waraka ukitoka haikuona
cha kujibu zaidi ya kuwatakia tu waumini kheri ya Pasaka.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments