Naibu wa rais wa Kenya William Ruto NAIBU rais wa Kenya,William Ruto,ameitaka tume ya uchaguzi ya Kenya kutaja rasmi siku ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo. Hatua ni baada ya Ijumaa mahakama ya juu zaidi kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita,ikisema kulikuwa na dosari kubwa zilizokiuka katiba ya Kenya. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyeusifu uamuzi huo wa mahakama,papo hapo alishutumu vikali tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC na pia kuwalaumu waangalizi wa kumataifa kwa kile alichokitaja ' kuhalalisha udanganyifu uliotokea na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike. Amewataka waliohusishwa na udanganyifu huo kujiuzulu , kufutwa kazi na hata kuchukuliwa hatua za kisheria wakisema kamwe hawawezi kuaminiwa kusimamia uchaguzi ujao. Rais uhuru Kenyatta akiwahutubia wafuasi wake jijini Nairobi. Alisema kuwa majaji waliobatilisha uchaguzi wkeni ni wakora Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta amesema ...