WANAFUNZI 7 WAFARIKI DUNIA BAADA YA BWENI LAO KUTEKETEA KWA MOTO NCHINI KENYA-Septemba 2
Waziri wa elimu Nchini Kenya Fred Matiang'i amesema kuwa
wanafunzi wengine 10 walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini ambapo kwa mjibu wa madaktari
nchini humo wawili kati ya hao 10 wako
katika hali mbaya huku wengine wanane hali zao zikiendelea vizuri.
Wakati huo huo kitengo cha habari cha maafisa wa msalaba
mwekundu katika shule hiyo kimesema takriban wanafunzi 10 hawajulikani waliko ambapo
kufuatia hali hiyo shule hiyo imefungwa
kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo
ambapo tayari kundi la wataalam wa upasuaji ikiwemo madaktari wako katika shule
hiyo kubaini chanzo.
Waziri Fred Matiang'I hata hivyo amesema wanafunzi wa kidato
cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa
kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajiandaa kufanya mtihani wa kidato cha
nne wa KCSE.
Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi wa
kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu
kujinusuru mbalii huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni hilo.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com
Comments