WAFANYABIASAHARA WA MITUMBA WALAANI KUONDOLEWA KWA NGUVU KATIKA SOKO LA MPANDA HOTEL-Septemba 2,2017
WAFANYABIASHARA wa mitumba katika
soko la Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelaani kitendo cha
kutaka kuondolewa katika maeneo ya biashara zao kwa kinachodaiwa kuwa
hawaruhusiwi kufanya biashara katika eneo hilo.
Wakizungumza baadhi ya
wafanyabiashara hao wamesema kuwa wao hufanya biashara katika eneo
waliloelekezwa na mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda hivyo wanashangazwa na
kitendo cha migambo kufika katika eneo hilo leo asubuhi na kuwataka kuondoka katika eneo hilo.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa
soko hilo Bw. Elisha kangombe amesema anashanga zwa na kitendo hicho na kusema
kuwa yeye kama kiongozi hakubaliani nacho.
Aidha makamu mwenyekiti huyo amesema kama
uongozi unalenga kuwaondoa wafanyabiashara hao ni vyema kuwaondoa wote bila
kufanya ubaguzi na kuwatafutia maeneo mbadala ya kufanya biashara zao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments