RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA NA WAUMINI KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO-Septemba 2,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo wameungana na waumini wa Kanisa la
Waadventista Wasabato,Usharika wa Magomeni Mwembechai Jijini Dar es Salaam
kusali Ibada ya Sabato.
Ibada hiyo
imeongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania,Baba
Askofu Mark Walwa Malekana aliyekuwa pamoja na Askofu wa Jimbo la Mashariki
Kati,Baba Askofu Joseph Mgwabi na Askofu wa Jimbo la Kusini Mashariki,Baba
Askofu Albert Nziku.
Akizungumza
baada ya Ibada hiyo Mhe.Rais Magufuli amelipongeza Kanisa hilo kwa kutoa huduma
ya kiroho kwa waumini wake na pia kutoa huduma za kijamii katika maeneo
mbalimbali nchini na amewahakikishia waumini na viongozi wake kuwa Serikali
inatambua mchango huo na itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini
katika kuwahudumia wananchi.
Wakati huo huo Mhe.
Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 na mifuko 400 ya saruji kwa ajili
ya ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato Usharika wa Magomeni
Mwembechai.
Aidha pamoja na kuchangia Shilingi Milioni 1 kwa kwaya za Kanisa
hilo na pia ameendesha harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa Kanisa na
kufanikisha kupata zaidi ya Shilingi Milioni ishirini na tano.
Kwa upande wake Baba Askofu Mark Walwa Malekana amemshukuru Mhe.Rais
Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya Sabato na
kuchangia ujenzi wa kanisa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments