MH.LOWASSA ATOA POLE KWA RAIS UHURU KENYATTA MAHAKAMA KUFUTA USHINDI WAKE-Septemba 2,2017
Mh.Edward Lowassa |
Mjumbe wa kamati kuu ya (CHADEMA) na Waziri Mkuu mstaafu Edward
Lowassa ametoa pole kwa aliyekuwa Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta kufutia
mahakama ya juu nchini humo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Urais uliofanyika
Agosti 8 mwaka huu.
Mhe.Edward Lowassa amesema yeye bado ataendelea kumuunga mkono hata
katika uchaguzi ujao kwa kuwa Uhuru Kenyatta ni kiongozi mwenye kusimamia
Demokrasia na mwenye maono ambaye anaweza kuisadia Kenya.
Aidha Lowassa amesema kuwa anamuheshimu sana Uhuru Kenyatta
kutokana na jinsi ambavyo anaheshimu Demokrasia na kudai katika kipindi chake
cha uongozi siku zote amekuwa akilinda Demokrasia ya nchi hiyo na kufanya
wabunge,vyama na kila mtu nchini humo kuwa na haki.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments