TRA MKOANI RUKWA YASAKA MAPATO KWA UDI NA UVUMBA YASHTUKIZA UKAGUZI WA MAGARI HASA YA MIKOANI-Septemba 2,2017-
MAMLAKA ya mapato TRA mkoani Rukwa imefanya
msako maalumu kwa lengo la kukagua mabasi ya abiria pamoja na ya mizigo ambayo
haijalipiwa kodi mbalimbali.
Akizungumza jana wakati akiongoza msako huo,Meneja msaidizi idara ya
ukaguzi wa TRA mkoa huo,Amina Shamdas amesema mamlaka hiyo inashirikiana na
kampuni ya Yono Auction Mart kufanya ukaguzi huo.
Amesema mamlaka hiyo imebaini wafanyabiashara wa usafirishaji
wamekuwa hawadai lisiti zinazotolewa na mashine za EFD wakati wakinunua mafuta huku
Magari mengi yakiwa na stika za za kughushi za kulipia Mapato.
Kwa upande wake David Philipo ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya
Yono Action Mart ya mjini Sumbawanga amesema wamekuwa wakikutana na changamoto
kubwa kutoka kwa wafanyabiashara hao ambapo baadhi yao wamekuwa ni wakaidi
katika kutii sheria.
Comments