WAZIRI MKUU AWASILISHA TAARIFA YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA SERIKALI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mpa akufikia Februari 2018 Serikali ya Awamu ya Tano imeanzisha viwanda vipya 3,306. Ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma,wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.