RC KATAVI AZINDUA VIKAO VYA KIELIMU ATOA MAAGIZO KWA WARATIBU WA ELIMU
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali
Mstaafu Raphael Muhuga,amewaagiza viongozi mbalimbali wa elimu mkoani Katavi kuhakikisha
wanashirikiana na wadau wa elimu katika maeneo yao ili kutatua tatizo la Mkoa
wa Katavi kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa kwa elimu ya msingi,kidato
cha nne na sita.
Miongoni mwa viongozi ambao
wamelengwa na agizo la Mkuu wa Mkoa ni pamoja na waratibu elimu kata,wakuu wa
shule,walimu wakuu,bodi na kamati mbalimbali za shule.
Muhuga ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa
agizo hilo wakati wa uzinduzi wa vikao vya wadau wa elimu Mkoani Katavi
uzinduzi ambao umefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Azimio Manispaa ya
Mpanda na kuhudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 1000,taasisi mbalimbali binafsi,wazazi,walezi
na wakuu wa idara Mkoa na Manispaa ya Mpanda.
Awali akiwasilisha taarifa kwa mgeni
rasmi,Kaimu katibu tawala Mkoa wa Katavi Ernest Hinju ambaye pia ndiye Afisa
elimu Mkoa amesema vikao hivyo vinavyoratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
vinalenga kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazosababisha ufaulu wa
wanafunzi kuendelea kuporomoka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Michael Nzyungu amesema
halmashauri inaendelea inaendeklea kutatua changamoto mbalimbali za kielimu
katika Manispaa ya Mpanda ikiwemo ukarababti na ujenzi wa miundombinu ya shule
kama madarasa ambapo mpaka sasa vyumba vya madarasa viapatvyo 26 vipo katika
hatua mbalimbali za kukamilika katika shule zenye uhaba wa madarasa.
Nao wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi,wazazi,walezi,
walimu,taasisi binafsi,viongozi mbalimbali wa dini na siasa ambao wameshiriki
katika uzinduzi wa vikao hivyo wamesema ili mkoa wa Katavi ufanye vizuri katika
mitihani ya taifa,inatakiwa kuwepo madarasa ya kutosha shuleni,stahiki
mbalimbali za walimu kulipwa kwa wakati,watoto kulelewa katika maadili mema na kuongezwa
idadi ya walimu shuleni.
Vikao hivyo vinatarajiwa kuwa saba
ambapo vitafanyika katika halmashauri za Mlele,Nsimbo,Mpimbwe,Mpanda na Manispaa
ya Mpanda ambapo kilele cha vikao hivyo kitafanyika Aprili 16 mwaka huu katika kijiji
cha majimoto Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlelele.
Mkoa wa Katavi kwa mwaka 2014,2015 na
2016 ulikuwa ukishika nafasi tatu za juu kitaifa kwa mitihani ya shule za
msingi na sekondari lakini kwa matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2017
umeporomoka na kushika nafasi ya 9 kitaifa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments