HIVI TANZANIA TUNAKOELEKEA NI WAPI?KIONGOZI WA WANAFUNZI TANZANIA ABDUL NONDO NAYE ATOWEKA
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umesema mwenyekiti wake Mahmud Abdul Ormari Nondo hajulikani alipo na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha anapatikana akiwa salama kwa haraka. Baba mdogo wa kiongozi huyo Mussa Mitumba akiwahutubia wanahabari pia ametoa wito kwa 'mwanawe' kurudishwa akiwa hai aendelee na kutafuta kutimiza ndoto zake. Abdul Nondo alituma ujumbe wa mwisho kusema alikuwa hatarini Kiongozi huyo wa wanafunzi alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo,Tahliso. Muungano huo unasema baada ya kuondoka afisi hizo,Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale. "Ghafla katika hali ya kutatanisha, kuanzia saa 6 hadi saa 8 usiku alijitoa kwenye makundi yote ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp jambo lililozua taharuki miongoni mwa watu wengi na kuanza kutaka kujua nin...